MAKALA

Karibu mpendwa msomaji katika ukurasa huu.

MAKALA ni ukurasa maalumu katika blogu hii kwa ajili ya kukupa darasa mbalimbali haswa zile za kiuchumi kijamii na hata kisiasa.

Ukurasa huu umejikita zaidi katika kubadilishana mawazo na mtazamo juu ya mustakabali wa maisha yetu ya kila siku na pirikapirika za utafutaji.

Ukurasa huu tutaanza kuufungua kwa kuangazia suala zima la ajira na yatokanayo na ajira.

AJIRA
Ni kazi ya halali iliyokubaliwa na kusimamiwa kwa mujibu wa sheria na jamii husika ambayo mtu huifanya na humpatia kipato.

Mfumo wa ajira umezigawanya ajira katika aina kuu mbili nazo ni ;- Ajira ya kujiajiri ;- Ajira ya kuajiriwa

Ajira ya kujiajiri
Hii ni aina ya ajira ambayo mtua anakuwa amebuni mradi wake wa biashara unaomuingizia kipato katika kuendesha maisha yake ya kila siku.Ajira hii aliyejiajiri huwajibika kujisimamia na kujituma kwa kuifanya kazi yake mwenyewe kuhakikisha anafikia malengo aliyojiwekea.

Ajira ya kuajiriwa
Hii ni aina ya ajira ambapo mtu anatoa muda na ujuzi wake katika kutumika au kutumikia kazi ya mtu mwingine kwa ajli ya kulipwa ujira wa mshahara au kibarua ili aweze kupata kipato cha kila siku cha kuendesha maisha yake.

Sekta za ajira
Ajira inaweza kutazamwa katika sekta kuu mbili katika jamii kulingana na usimamizi.Kuna ajira ya sekta binafsi na ajira ya utumishi wa serikali

Ajira ya sekta binafsi
Hii ni aina ya ajira ambayo taasisi au mashirika na hata kampuni zisizo za kiserikali huajiri watu wa fani mbalimbali kwa ajili ya kutumika kwenye mambo mbalimbali ya uzalishaji mali.Malipo ya walioajiriwa huwa ni mshahara au ujira wa kibarua katika muda unaokubalika kisheria.Ajira binafsi huwa na kada kuu mbili waliojiajiri na walioajiriwa.

Ajira ya utumishi wa serikali
Hii ni aina ya ajira ambapo serikali huajiri watumishi katika kuendesha idara,mamlaka na hata mashirika mbalimbali ya serikali kwa muktadha wa malipo ya mshahara ifikapo mwisho wa mwezi.

Ajira katika nchi
Katika nchi yoyote ile suala la ajira ni la lazima madam mtu amefikia umri wa miaka 18 kisheria, na kama si mwanafunzi anaweza kufanya kazi na kuingia mikataba mbalimbali katika suala la uzalishaji mali na kupata kipato cha kujikimu.

Utaratibu wa ajira katika nchi yetu ya Tanzania husimamiwa na sheria za nchi yaani sheria ya kazi.Muajiriwa awe ni mtumishi wa uma au sekta binafsi atatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za kazi na hata muajiri hali kadhalika atatakiwa kuhakikisha katika eneo lake la kazi anazifuata sheria zote za kazi.

Ajira ni suala muhimu sana kwa kila binadamu kwa ajili ya kuweza kupata kipato cha kujikimu mahitaji yake ya msingi ya lishe, mavazi na malazi.

Binaadamu ameumbwa kufanya kazi ili aweze kupata mahitaji yake ya msingi hakuumbwa kuwa goigoi.Kazi hii si tu iwe inatimiza matakwa na taratibu za nchi pia iwe inapendeza mbele ya mola na macho ya jamii inayokuzunguka.

Binaadamu ameumbwa akapewa tunu zifuatazo:-
AFYA , AKILI, KIWILIWILI.Binaadamu aliyetimia katika hayo anatakiwa  kujuwa hiyo ni neema ya mola wake anatakiwa aitumie kuzalisha mali kwa ajili yake na kuisaidia jamii iliyomzunguka haswa wale ambao hawajiwezi kwa maana hawakubahatika kupata tunu hizo.

Tumeletwa dunia kumuabudu mungu na pia kufanya kazi ili kuweza kutimiza mahitaji ya msingi ya kuishi.Tumeumbwa tofauti tofauti ili tuweze kutegemeana na kwenye kutegemeana na kusaidiana ndiko mapenzi na upendo kwa wanaadamu hujengeka.

Unapofanya kazi na kupata kipato chako kumbuka humo kwenye kipato chako kuna fungu la masikini na mafukara na wasiojiweza wanatakiwa kusaidiwa.

Sio uwasaidie kwa kuwapa hela tu, hapana , unatakiwa pia uwasaidie kwa kuwajengea  uwezo na kuwawezesha nao wakazalishe mali.

Ukiendelea kumsaidia kwa kumpa hela na anao uwezo wa kuzalisha mali kwa kuzingatia tunu alizotunukiwa na mola basi jua unaidumaza akili yake na kuua uwezo wake wa kufikiri.Msaidie kumuonesha kuwa anao uwezo wa kujikimu hapo mjengee uwezo.Kesho na yeye atatafuta, na atasaidia wengine kwa namna hiyo.

Suala la ajira limekuwa ni kilio kikubwa sana kwa jamii,Akisimama mwanasiasa utamsikia analalamika kuwa watu hawana ajira.Akisimama mchumi atasema watu hawana ajira viongozi wa dini watasema nao watu hawana ajira ilimradi tu kila mtu aoneshe suala la kutokuwa na ajira ni jambo kubwa sana.

Makala hii itajadili kwa kina suala la ajira na litakuelezea na kukuonesha tatizo sio watu hawana ajira bali ni mtazamo.Kila anayelalamika kuwa watu hawana ajira jua fika humaanisha ajira ya kuajiriwa umtumikie mtu akulipe mwisho wa mwezi au serikali ikulipe mwisho wa mwezi.

Tatizo la mtazamo hapa ni "upofu" yaani wameangazia kuwa ajira ni ile tu iliyokuwapo kwenye mfumo rasmi na vijana wote wameelekeza akili zao huko na ukiwauliza wanasema na wao nimesoma mpaka leo sina kazi.

Haya ni maajabu katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.

Hebu turejee kisa hiki cha binaadamu wa kwaza kuwapo duniani ambaye ni NABII ADAMU 

Nabii Adamu aliumbwa na mungu akaletwa duniani kuja kuishi yeye na Hawa.Mungu wakati anamleta duniani alishamuwekea adamu rasilimali zote na alipomuumba alimpa elimu ya muongozo na mazingira ili kuweza kuyatawala maisha yake ya hapa duniani katika kutumia rasilimali mbalimbali kuweza kujikimu na kupata radhi za mola.

Hivi adamu alipewa elimu kisha akaletwa duniani na akayahimili mazingira akaanza kula matunda akajifundisha kuwinda kulima na hatimaye baba yetu ADAM na mama yetu HAWA wakaujaza ulimwengu.

Hivi hawa nao wangeanza kulalamika kumlalamikia mungu hali ingekuaje? 

Kijana msomi ambye unakesha na kusoma na kuhangaika kupekua kwenye mitandao ya kijamii elewa hili.Suala la kusoma ni jambo la msingi sana kwa kuwa linakujenga na kukuza upeo wa akili yako uweze kufikiri vyema na kuweza kuzikabili changamoto za kilimwengu katika mazingira yako ya maisha ya kila siku.Elewa kuwa jukumu la serikali na sekta binafsi si kukuajiri wewe ukiajiriwa hiyo ni bahati itumie vyema.

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi jukumu lake ni kuweka miundo mbinu mizuri ya rai kupata elimu.Raia anyepata elimu anatakiwa sasa atumie akili na kipawa chake kubuni njia sahihi na za halali za kujizalishia mali.

Nje ya elimu bado una akili yako yenye uwezo wa kung'amua mambo anuai na maarifa tele ya kuweza kubuni miradi midogomidogo ya kukuzalishia mali na kuendeleza maisha yako.

Ukiitumia akili yako vizuri kutafakari hutakaa ukisubiria ajira ya kuajiriwa haraka sana utapata wazo la kuweza kujiajiri.

Ukizungumza haya utasikia mwingine anakuja na hoja kweli maneno yako ni sawa tatizo ni mtaji.

Mtaji? hebu nenda katafakari kisa cha nabii ADAMU je mtaji kwake ulikuwa ni hela? mbona ukiwaza mtaji unawaza hela? Baba yetu ADAMU alipoletwa ulimwenguni alianzaje na alianzia wapi kivipi katika kuchuma na kujikimu? 

Nakuacha na tafakuri na nitarejea tena........mungu akipenda

Amarison tupo kwa ajili ya kukuzindua.

KUTOKUWA NA AJIRA SIO TATIZO NI MATOKEO YA KUWA NA "MTAZAMO POFU" 

Tembelea:  www.amarisontanga.blogspot.com






No comments:

Post a Comment