HUDUMA ZETU


Karibu mpendwa msomaji

AMARISON hutoa huduma zifuatazo:

Real estate

Hii ni huduma pana sana na ina mambo mengi kuhusiana na mali zote zitokanazo na ardhi,AMARISON imejikita kwenye uwakala wa kuuza mashamba,nyumba na viwanja.

AMARISON hawana kiwanja wanachomiliki bali wao ni wakala tu wa kuuza kiwanja,shamba ,nyumba kutoka kwa mmiliki husika katika makubaliano maalumu ya malipo.

Tunapokea nyumba ,viwanja na mashamba kisha tunayatafutia wateja wanaohitaji kununua.Hapokei kitu chenye mgogoro,kujenga uaminifu kwa wateja wetu tunahakiki mali tunayopewa katika mamlaka husika kabla ya kuiuza.

Unapohitaji huduma hii gharama yake kubwa ni kulipia shilingi 10,000/= ya kitanzania na utapelekwa kwenye viwanja kulingana na hitajio lako.Gharama hii itakufikisha kwenye kata tano tu za Tanga jiji ulizochagua na si zaidi.Hakuna gharama utakazolipia zaidi ya hizo

Kwa kununua kiwanja chenye uhakika bila ya mgogoro wasiliana nasi kwa simu +255678134834

Property Management

Hii ni huduma inayohusu usimamizi wa miradi mbalimbali.
AMARISON imejikita kwenye kusimamia ukusanyaji wa kodi za pango husika kutoka kwa wapangaji kwa kuidhinishwa na mmiliki.Katika huduma hii AMARISON huingia mkataba maalumu na mmiliki na namna ya kulipana katika kufanikisha kazi hiyo.

Epuka usumbufu kwa wapangaji tukabidhi kazi yako tutakufanyia kwa ufanisi na kwa mujibu wa sheria wasiliana nasi kwa simu +255678134834

Ujasiriamali

Hii ni huduma pana sana.AMARISON tumejikita zaidi katika kutoa mafunzo mbalimbali yanayomsaidia mtu kumjengea uwezo wa kuzibaini fursa na namna ya kuziendea katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa ajili ya kukuza kipato.

Mafunzo haya hutolewa kwa watu wa kada zote.Mahali ulipo wewe na wenzako mnaweza kujiratibu na tukaja kuwapa mafunzo.Kwa masaa kila mtu atalipia shilingi 10000/= ya kitanzania.Mafunzo haya kwa gharama hii ni ndani ya jiji la Tanga na kwa watu kuanzia watano.

Hujachelewa wakati ndio huu wasiliana nasi kwa simu +255678134834

Marketing

Hii ni huduma ya kutafuta bidhaa masoko.AMARISON tumejikita zaidi katika kuhakikisha bidhaa zako zinapata soko na pia kukupa ushauri wa kitaalamu wa namna ambavyo unaweza kutumia mbinu mbalimbali za masoko na ukafanikiwa kuuza bidhaa zako hatimaye ukaongeza mauzo.

Hujachelewa sasa kuongeza mauzo yako wasiliana nasi kwa simu +255678134834

Insurance

Hii ni huduma inayohusu masuala ya bima.AMARISON tumejikita zaidi katika kutoa elimu juu ya bima na mahitaji ya bima na pia kushauri kufuatilia madai ya bima.Kwa kushirikiana na kampuni pamoja na mawakala mbalimbali unaweza kupatiwa huduma hii.

Kwa ushauri juu ya bima wasiliana nasi kwa simu +255678134834

Education management

Hii ni huduma inayotolewa na AMARISON kuhakikisha inakupa ushauri wa kutosha katika kuendesha kituo cha elimu kwa ufanisi zaidi na wenye tija.

Katika huduma hii AMARISON imejikita zaidi katika ukaguzi wa vituo vya elimu,utawala wa kituo cha elimu ,na kutoa mafunzo maalumu kwa wanafunzi na wakufunzi ya namna gani wanaweza kukuza maendeleo na ufanisi wa kituo husika cha elimu.

Hujachelewa wahi sasa kwa kuboresha kituo chako cha elimu tafadhali wasiliana nasi kwa simu +255678134834

Advertisement

Hii ni huduma inayohusika na uandaaji na utengenezaji wa matangazo ya biashara kwa njia ya redio televisheni na mitandao ya kijamii.

Je unabiashara yako unahitaji kuitangaza? wasiliana na AMARISON tutakupa ushauri na namna ya kuitangaza biashara yako kwa mafanikio.

Tafadhali kwa matangazo ya biashara wasiliana nasi kwa simu +255678134834

Tourism information centre

Hii ni huduma inayohusika na kutembelea katika maeneo mbalimbali ndani ya jiji la Tanga kwa ajili ya kutalii pamoja na mkoa wa Tanga kwa ujumla wake.

Vipo vivutio vingi vya utalii ndani ya mkoa wa Tanga lakini wengi hawavifahamu.AMARISON tupo kwa ajili ya kukuonesha vivutio hivyo vya utalii na kufurahia maisha ya Tanga.

Hujachelewa nafasi ni sasa wasiliana nasi kwa simu +255678134834

Information and communication technology

Hii ni huduma pana sana ambayo inahusu masuala mtambuka ya mawasiliano.AMARISON itakuwezesha kuweza kupata huduma za;

Huduma za kisasa za kisayansi katika usimamizi wa kituo cha kazi kwa upande wa wafanyakazi na taarifa mbalimbali za kazi.

Huduma hii pia itakuwezesha kuweza kupata ujuzi na weledi wa kubadilisha kituo chako cha mawasiliano ya redio au tv kuwa na muenekano bora na kuandaa program zinazokidhi mahitaji ya wakati husika kwa utaalamu wa hali  ya juu.

Kupitia huduma hii tunatoa ushauri katika usimamizi wa vituo vya idhaa za redio ,televisheni kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kuwapa mafunzo wafanyakazi husika kuendana na wakati.

Haujachelewa katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia wasiliana nasi kwa simu +255678134834 .

Endelea kutembelea blogu yetu kwa mafunzo zaidi.
No comments:

Post a Comment