Thursday, 20 October 2016

MIKOPO ELIMU YA JUU

Nawashangaa watanzania

MTU anasomesha mtoto ada milioni 3

Analalamika kukosa mkopo wa 1.5 m kulipia ada ya chuo kwa MWAKA

Watu wanailaumu serikali eti wanafunzi wamekosa mikopo bali hawalaumu waliokopeshwa kuingia mitini kutokulipa

Wanasingizia hawana ajira wakati kuna kujiajiri na kwa mwezi unatakiwa kulipa kima cha 50000 kwenda juu hiki ni kiwango nilichokuwa nikilipa deni langu la bodi ya mikopo sijui sasa kima cha chini ni kiasi gani.

Hukusoma ili uajiriwe umesoma ili uondoe ujinga na upumbavu hatimaye ujiajiri.  uendeshe maisha yako na ulipe deni la mkopo wa elimu ya juu.

Ni ujinga wa hali ya juu kusema wanafunzi 66000 wa elimu ya juu wamekosa mikopo

Wakati kuna vijana zaidi ya milioni toka 1994 mpaka 2015 hawajalipa hata shilingi wanadaiwa .

ILI WATANZANIA WENGINE WAWEZE KUKOPESHWA KUSOMA ELIMU YA JUU

WEWE ULIYEMALIZA MWAKA 1994 HADI 2015 LIPA ILI WENGINE WAKOPESHWE.

Kwanza jamii yetu ishajitenga siku nyingi eti wanaosoma shule za serikali ni masikini na wanaosoma shule za kulipia ni matajiri.

Katika msingi huu wanaomaliza Shule za serikali nashauri wapewe kipaumbele kwenye mikopo maana hawana uwezo.

Serikali na bodi ya mikopo nashauri kigezo kimojawapo cha kupata mkopo wa elimu ya juu iwe ni kuangalia anayeomba amehitimu elimu Yake Wapi

Shule ya msingi

Shule ya sekondari

Kidato cha sita

Maaana kuna wanaolipa milioni 4 kusomesha  chekechea eti na wao wapewe mikopo kwa kuwa wana watoto elimu ya juu alaaaa

Dahh ningekuwa nina mamlaka ya mwisho

Ningehakikisha aliyesoma Shule ya msingi ya serikali la kwanza hadi la saba pamoja na sekondari ya serikali na kidato cha sita kahitimu Shule ya serikali hakika huyu angepata mkopo 100%

Hapa hakuna ubaguzi maana wakati wewe unasoma Shule ya mamilioni na mwingine anasoma shule ya elimu bure hukuuona huo ubaguzi ndio uje kuuona chuo kikuu kwa kuwa umekosa mkopo?

Kama uliweza kulipa malaki na mamilioni kuanzia shule ya msingi endeleaaa tu baba kulipa mamilioni elimu ya juu iweje ule ng'ombe mzima uahindwe mkia?

Kama kuna aliyesoma kwa ada ya chini ya laki moja elimu ya msingi mpaka kidato cha sita aendelee tu kusaidiwa na serikali kukopeshwa na kupata elimu ya juu maana huyu ndio hana uwezo.

KILA MBUZI ATAKULA KWA UREFU WA KAMBA YAKE.

Amarison
2016

Monday, 10 October 2016

TUMIA WAYA ZA MASTER CABLE KWA USALAMA WA JENGO LAKO

MASTER CABLE ni waya za umeme zenye kiwango na ubora wa hali ya juu uliotihibitishwa na TBS

Waya za MASTER CABLE zinatengenezwa nchini TANZANIA

Copper halisi yenye kiwango na ubora wa hali ya juu ndio inayotumika kutengeneza waya za MASTERCABLE

Ubora wa waya za MASTER CABLE umepimwa kwa kuzingatia viwango vyote vya ubora.

WAYA za MASTERCABLE zinapimwa katika uwezo wa kubeba mkondo wa umeme 3000VOLT ambapo umeme wa kawaida kwa matumizi ya kitanzania ni 250 volt .

Hiki ni kiwango bora kabisa cha kupima ubora wa WAYA DUNIANI katika kuhimili mkondo wa umeme hii inakuhakikishia kuwa hata kama umeme utazidi kwa ghafla hauna uwezo wa kuleta madhara ndani ya nyumba yako maana WAYA ZA MASTER CABLE zinauwezo mkubwa wa kuhimili mkondo wa umeme hata ule usio wa hali ya kawaida.

Tafadhali kwa USALAMA WA JENGO lako TUMIA WAYA ZA MASTER CABLE

Waya zetu ni

1.5 single

2.5 single

1.5 twin

2.5 twin

4 twin

6 twin

Waya za single kuna za red green na black

Plastic inayotumika kufunika waya yaani PVC kwa wale wasiofahamu ile ngozi ya juu ya waya ina ubora wa hali ya juu ambayo ina uwezo wa kuhimili joto kubwa sana bila kupata madhara.

PVC hujaribiwa kupitia kifaa maalum ambapo waya huingizwa katika kifaa hicho kikiwa na maji ya moto yenye nyuzi joto 70 na kupewa volt ya umeme 3000 kwa kuzingatia joto la maji na joto la mkondo wa umeme ndipo uimara wa PVC huthibitika. Hapa tunapima uwezo wa PVC kuhimili joto na kutokulainika .

Kwa kuzingatia haya ndipo tunathubutu kusema WAYA ZETU NI BORA NA ZINA KIWANGO KILICHOTHIBITISHWA NA TBS waya zetu ije jua ije mvua haziwezi kuleta madhara katika NYUMBA yako.

MASTER CABLE

"We are the master of cables in Tanzania"

Waya zetu zinapatikana katika maduka yote yenye vifaa vya umeme kariakoo DSM

Usinunue waya nunua MASTER CABLE

Bei za waya zetu utazipata madukani maduka ya jumla na rejareja kwa sasa waya zipo MADUKA YOTE KARIAKOO DSM na ARUSHA .

Kwanini uhatarishe usalama wa NYUMBA yako kwa kutumia waya zisizobora?

Waya zetu zote zipo katika ujazo wa 100m kwanini ununue waya pungufu wakati waya bora zipo?

Waya zetu za twin zina poda inayoimarisha na kuupa waya wetu kiwango cha kimataifa zaidi.

Usihangaike na bidhaa fake nunua waya wenye ubora.BEI ZA WAYA ZETU NI KWASABABU YA UBORA WETU

Wakati ni huu sasa TUMIA MASTERCABLE KWA USALAMA WA JENGO LAKO

Wakati ni huu

TUMIA MASTERCABLE KWA USALAMA WA JENGO LAKO

KUTOKUWA NA AJIRA NI TATIZO LA" MTAZAMO POFU"


Mtazamo pofu ni aina ya mtazamo ambao mtu anakuwa hana uwezo wa kuona jambo zaidi ya upeo wake wa ziada bali huweza kuliona jambo katika mtazamo mmoja tu.

Jamii na kila mwanajamii analalamika kuwa hana ajira.Kilio hiki ni kikubwa sana kwa vijana wasomi kwasababu wao wanaamini zaidi juu ya ajira ya kuajiriwa na si kujiajiri.

Iwapo utawahoji na kujadiliana nao juu ya ajira ya kujiajiri basi jambo moja kuu litakalokuwa kikwazo kwa vijana wasomi watakwambia hawana mtaji.Wakimaanisha mamilioni ya hela ya kuweza kufanya biashara.

Mtazamo pofu huanzia pale mtu anapoitazama ajira kuwa ni lazima uwe umeajiriwa sehemu fulani uko kwenye kiti cha kuzunguka una nesanesa na kupulizwa na kiyoyozi ila hana imani juu ya ajira ya kujiajiri.

Mtazamo pofu pia hujitokeza pale unapotazama mtaji kuwa ni hela ya kuanzia biashara huu nao ni mtazamo pofu maana umeshindwa kuweza kuona yaliyokuwepo zaidi ya hapo.

Angalia maisha ya vijana waliohitimu vyuo vikuu wanavyohangaika kutafuta kazi huku wakiwa tayari kichwani wana maarifa yenye nadharia nyingi na mipango mingi ya mafanikio ila wameshindwa kuamua kutekeleza kivitendo maarifa hayo ili yawapatie kipato.

Tazama vijana walioishia kidato cha 4 au cha 6 wako mtaani wakifanya biashara zao na wanaendesha maisha yao kwa ufanisi tu,  msomi ana hahaha mtaani kutafuta kazi huu ndio upofu.

Niliamua kuchukua muda katika maisha yangu kuanza kulifanyia utafiti haswa kwa hawa vijana ambao wao hawakufikia elimu ya juu ila  wengi wao ndio wafanyabiashara na ni wajasiriamali huku wasomi wakibaikia katika hatua ya kuajiriwa na hao na kulia njaa kila baada ya siku.

Kitu nilichokibaini ni kuwa, vijana hawa ambao hawakufika elimu ya juu wao wana uthubutu ujasiri subra na uvumilivu saana katika kuyaendea maisha yao na wana nidhamu kubwa ya matumizi ya pesa kwasababu wanajua ugumu wake na kupatikana kwake kwa namna wanavyoitafuta katika biashara zao za kila siku.

Kitu kingine ambacho nimekigundua kutoka kwa vijana ambao ni wafanyabiashara na hawakufikia elimu ya juu kuwa wao wanaishi maisha yao halisi si maisha ya kutaka kuonekana kuwa ni watu wa hali flani ya juu kimaisha ambapo matumizi yao yamekuwa ni ya wastani na muda mwingi hufikiria zaidi kuwekeza katika fursa nyingine za kibiashara.

Jambo la mwisho nililolibaini ni kuwa wao kila fursa wanaiona ni njia ya kuitumia kujipatia kipato cha halali.Nilipojaribu kuwahoji na kuuliza asilimia kubwa kati yao wakati nikiwauliza mwanzo wa biashara zao walinijibu uaminifu ndio mtaji wake alioanza nao ambapo mpaka leo analetewa mizigo anauza na kulipa kama kawaida.

Wakati msomi akihangaika na business plan na maandiko mradi kutafuta wadhamini na wahisani huku akiamini juu ya mtaji pesa tayari kuna ambao wao wameanza na mtaji uaminifu.

Yupo aliyenisimulia maisha yake kuwa yeye aliamua kuchukua bidhaa kwa mtu na kuanza kusambaza katika maduka na katika kila bidhaa aliyokuwa akisambaza yeye alikuwa akiongeza shilingi 1000 au 500 ambapo leo hii ana miliki duka kubwa sana la simu na vipodozi katikati ya jiji la Dar es salaam.

Kila ukimuuuliza jibu atakwambia kaka mimi sijasoma nimeishia kidato cha 4 ila uaminifu ndio umenifanya nimefika hapa.Hakika ukisikiliza historia zao watu hawa unaiona tofauti kubwa sana kati ya kijana msomi na kijana aliyeishia kidato cha nne katika uthubutu wa kujaribu na kujiajiri.

Duniani kote inaonesha dhahiri kuwa sekta ya ajira ya kuajiriwa iwe ni serikalini au sekta binafsi ni 25% tu kila mwaka wanaoajiriwa kutoka kwa waliohitimu katika kila nchi katika sekta zote.Je 75% inakwenda wapi? Hapa ndipo unapoiona sekta ya kilimo na ufugaji ikisubiri 75% sekta ya uvuvi ikisubiri 75% sekta ya ujasiriamali  na uchuuzi ikisubiri asilimia iliyobaikia.

Katika mazingira haya ndipo unapoona mtazamo pofu wa kuiona ajira ya kuajiriwa na kutokuiona ajira ya kujiajiri hatimaye kila msomi huililia serikali kutoa ajira.

JUKUMU LA SERIKALI dunia nzima ni kujenga miundombinu bora na imara ya raia wake kuweza kupata maarifa yaani elimu itakayowawezesha wao kuzikabili changamoto zilizopo katika mazingira yao na sio kuajiriwa.Ikiwa umehitimu shahada ya kwanza na mpaka leo unahangaika kutafuta ajira na huzioni fursa za wewe kujiajiri basi jua pamoja na elimu yako na wewe una mtazamo pofu.

Duniani hakuna serikali inayoajiri 100% katika 25% hugawana na sekta binafsi sasa wewe unayesubiria kuajiriwa utasubiri sana maana wapo wengi kama wewe wanaendelea kulia na kusota mtaani wamebakia kujisifu kuwa wamesoma sana.Wamebaikia na vyeti wakiviangalia kama picha na kuvisoma kama magazeti.

Acha kujidanganya na hivyo vyeti sekta ya kujiajiri haingalii mivyeti yako inaangalia upeo na akili yako ya kuweza kuyaona maisha nje ya mtazamo wa darasani ulipokuwa ukisoma.

Ukitaka kujiajiri sahau kwa mda habari za degree yako huku mtaani kwenye kujiajiri hiyo haina nafasi kwa mwanzo utakuja kuitumia mbeleni.Ile elimu uliyoipata ambayo ipo kichwani kwako ndio sasa inatakiwa ikuoneshe namna gani unaweza kuziona fursa na kuziendea.

kumbuka : HUSOMI ILI UAJIRIWE UNASOMA KUFUTA UJINGA NA UPUMBAVU ili uweze kupata maarifa yatakayokuwezesha kukupa mbinu bora ya kuzikabili changamoto za maisha yako.

KAMA ULISOMA KWA MTAZAMO HUU WA KUAJIRIWA UJUE UNA MTAZAMO POFU

Makala hii ni kwa ajili ya wewe ambaye mpaka leo unasubiri kuajriwa.

NINI CHA KUFANYA kuondokana na mtazamo huu pofu endelea kufuatilia

www.amarisontanga.blogspot.com 

kwa elimu zaidi.