Saturday, 11 March 2017

TANGA NA FURSA YA UWEKEZAJI

Mkoa wa Tanga ni mkoa uliosheheni kila aina ya fursa ya kiuchumi kutokana na miundombinu yake inayopelekea maeneo mengi kufikika kwa urahisi.Pia mkoa huu unapakana na nchi jirani ya Kenya kupitia mji wa Mombasa unaoifanya Tanga izidi kuwa sehemu nzuri ya kuwekeza na hata kusafirisha bidhaa mbalimbali nchi jirani na kujipatia fedha za kigeni.

Mkoa wa Tanga umejaaliwa kuwa na bahari ya hindi ambayo ni fursa nyingine ya kusafirisha bidhaa mbalimbali nje ya nchi hususan nje ya Afrika Mashariki.Uwepo wa bahari ni neema kubwa kwa watu wa Tanga na uchumi wa mji huu.Bahari huwezesha meli kusafirisha mizigo na bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Iwapo uchumi wa bandari utakuzwa kwa kiwango cha hali ya juu na kuwa na bandari ya kubwa na ya kisasa milango ya uchumi wa Tanga itazidi kufunguka maana itakuwa ni kiunganishi kikubwa hata na nchi za Ulaya na za Asia.

Nchi nyingi duniani zilizokuwa na bahari na kuamua kuwekeza kwenye uchumi wa bandari hakika zimewafugulia milango katika kukuza sekta ya uchumi wa viwanda na hata biashara pamoja na sekta ya utalii.

Hapo awali mji wa Tanga ulisifika sana kwa uchumi unaoliendesha Taifa la Tanzania hususan kwenye sekta ya kilimo cha mkonge na korosho halikadhalika katika upande wa viwanda mji wa Tanga ndio ulikuwa gwiji katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo,usindikaji wa matunda ,maziwa,chuma,saruji,bidhaa za viuongo mbalimbali.Kiukweli ukielezea historia ya mji wa Tanga kiuchumi unaweza kutoka machozi maaana yale yote yaliyoiletea sifa Tanga na Tanzania ndani ya mji wa Tanga leo yamekuwa ni magofu na magereji na hali ya uchumi wa viwanda umekuwa kizungumkuti.Hakuna mtanzania asiyeijua Tanga na uchumi wake ulivyokuwa ukiiendesha Tanzania.

Hiyo ni historia haina maana historia iachwe ipite tu lahasha historia pia hutukumbusha kuwa inatabaia ya kujirudia.Sasa ni zemu yetu Tanga kuchanua kwa uchumi wa bandari viwanda na biashara.

Iwapo wana Tanga wenyewe hawataamka na kuhamasisha juu ya fursa za uwekezaji zilizoko ndani ya mji wa Tanga wawekezaji wengi katika sekta mbalimbali watavutika na kuja kuwekeza.Kuna uwezekano mkubwa tu wapo wanaotaka kuwekeza Tanga bali hudanganywa au hata kutishwa na baadhi ya watu tu eti Tanga hakuna mzunguko wa hela utapata taabu.Dhana hizi haziwezi kubadilishwa kama wana Tanga tutakaa kimya juu ya Tanga yetu.

Zamu yetu sasa kuirejesha heshima na hadhi ya Tanga makampuni mbalimbali yameonesha nia na dhamira ya kuja kuwekeza Tanga wakati ndio huu wa kupambana kutangaza fursa zote zile za uwekezaji ndani ya mji wa Tanga na wilaya zake.

Tanga ni zaidi ya dhahabu lulu au almasi ina neema za kila aina na utajiri mkubwa wa rasilimali za kila aina wakati ndio huu tuhamasishane kuwekeza ndani ya Tanga kwa kuzielezea fursa mbalimbali za uchumi ndani ya mkoa wa Tanga.

AMARISON CONSULTANCY tumeanza kuitangaza TANGA NA FURSA ZA UWEKEZAJI na wewe tumia fursa yako kuitangaza TANGA.

TANGA KWANZA

Usikose toleo lijalo tutaanza na WILAYA YA MKINGA NA FURSA YA UWEKEZAJI

No comments:

Post a Comment